Diamond, Nay wa Mitego na Alaine wa Jamaica waingia studio kutayarisha wimbo

Haijulikani ni nani amemshirikisha nani lakini kuna uwezekano mkubwa Alaine amemshirikisha Diamond.
Nay wa Mitego ameshare picha Instagram akiwa studio na Diamond, Alaine, Tudy Thomas, meneja wa Diamond, Sallam na wengine.
Alaine amekuja Afrika Mashariki wiki iliyopita na anatarajiwa kuzindua album yake mpya nchini Kenya.
Hii ni mara ya pili muimbaji huyo anakuja nchini. Mwaka 2013 alikuja kwenye Fiesta ya Dar es Salaam.
No comments