TETESI: ZLATAN IBRAHIMOVIC KUTUA OLD TRAFFORD KAMA KOCHA MSAIDIZI WA MOURINHO
Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden ataondoka Paris Saint-Germain kwenda Manchester United ili kuwa kocha msaidizi wa Jose Mourinho
Zlatan Ibrahimovic yupo mbioni kutua Manchester United kuwa kocha msaidizi wa Jose Mourinho anayetarajiwa kuwa meneja wa klabu hiyo kwa mujibu wa chanzo cha Sweden Aftonbladet.Mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden ataondoka Paris Saint-Germain majira haya ya joto na Manchester United ndio wanaopewa nafasi kubwa kuipata saini yake. Kama habari hizi ni za kuaminika Ibrahimovic atakuwa moja ya wakufunzi katika benchi la ufundi litakalokuwa chini ya Jose Mourinho.
No comments