Breaking News

TETESI: VAN GAAL & MOURINHO KUFANYA KAZI PAMOJA MSIMU UJAO

Mreno huyo amedumu kwa miezi sita bila kazi kufuatia kutupiwa virago Chelsea lakini anatazamiwa kurejea tena kazini kushirikiana Louis van Gaal Old Trafford.
Louis van Gaal anatarajiwa kupewa kazi ya Mkurugenzi wa soka Manchester United ili kutoa nafasi kwa Jose Mourinho kuwa meneja mpya wa klabu hiyo katika kampeni za 2016-17, kwa muhibu wa The Sun .
Wawili hao wana uzoefu wa kufanya kazi pamoja walipokuwa Barcelona miaka ya 1990, na makamu mwenyekiti wa United Ed Woodward bado anataka kuendelea kuutumia uzoefu wa Mdachi LVG kuifaidisha klabu.
Pia Mourinho amekataa ofa kutoka kwa klabu nyingine pinzani ili kupata fursa ya kutua Old Trafford baada ya kufukuzwa Chelsea kwa mara ya pili Desemba mwaka jana.

No comments

Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!